ARSENAL, ikicheza Ugenini huko KP Stadium na Timu iliyopanda Daraja Msimu huu Leicester City, imetoka Sare ya Bao 1-1.
Arsenal ndio walitangulia kufunga kwa Bao la Mchezaji wao mpya Alexis
Sancheza katika Dakika ya 20 laki Dakika 2 baadae Leicester
walisawazisha kwa Bao la Mchezaji wao mpya Leonardo Ulloa.
Hii ni Mechi ya pili mfululizo kwa Arsenal kutoka Sare kwenye Ligi
baada ya Wiki iliyopita kutoka 2-2 na Everton huko Goodison Park.