Waziri  Mwakyembe aliyasema hayo bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali  zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya wizara  yake.
"Tembea  dunia kote huko, nimekwenda Nigeria na kuona wasanii wakubwa kama Tiwa  Savage, Don Jazz, Akon, P Square wale hawaimbi kuhusu viongozi wao wa  kisiasa.
"Hivyo  niwasihi wasanii wangu, muache kuimba kuhusu siasa sababu hii ni  ‘entertainment industry’ (sekta ya burudani) na sio ya masuala ya  kisiasa, "alisema Waziri Mwakyembe.
Aidha,  waziri alisema kama kuna msanii yeyote anayetaka kuwa mwanasiasa aache  muziki akagombee udiwani kwani wasanii waliotaka kuchanganya siasa na  muziki walipotea kabisa.

