Mahakama
 Kuu ya Tanzania imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za 
Kiislamu nchihi, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na Jamhuri 
kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyokuwa imemuachia huru.
Mahakama
 chini ya Jaji, Johnson Mkasimongwa ambaye ameeleza kuwa anakubaliana na
 uamuzi wa Mahakama ya Morogoro ya kumuachia huru Sheikh Ponda katika 
kesi ya kutoa lugha ya uchochezi.
Jaji
 Mkasimongwa amesema Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru 
Sheikh Ponda na yeye anakubaliana na uamuzi huo, hivyo amechukua uamuzi 
wa kumuachia huru.
Akitolea
 maelezo juu ya maamuzi hayo, Jaji Mkasimongwa amefafanua  kwa kusema 
kuwa upande Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la 
kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika 
Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.
Sheikh
 Ponda alishtakiwa kwa tuhuma za uchochezi ambapo mnamo August 10, 2013,
 August 10, 2013, alidaiwa kutoa kauli za kichochezi kwa waumini wa 
kiislam ambapo moja ya kauli zake alisema kwamba (Waislam) wasikubali 
uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa 
zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

