Audio: Drake amshirikisha Rihanna kwenye "Views From The 6" azungumzia uhusiano waliokuwa nao

Wakati Drake aliposema “diss me, you’ll never hear a reply for it” 2009 kwenye "Successful" inaanza kuonekana ukweli wake kuwa alimaanisha hutaskia jina lako likitajwa.
Siku chache baada ya Rihanna kuhudhuria tua ya "Lil Wayne Vs Drake" Drake ameongelea uhusiano wao uliopita katika wimbo uliovujakwenye mitandao

Wakati wa tour ya Darke Europe "Would you Like a Tour?" mwishoni mwa mwezi wa pili, Rihanna ali-perform na Drake Paris, kisha wiki mbili baada ya hapo walionekana katika migahawa mbali mbali wakiwa wameshikana mikono na hata kuingia katika choo kimoja cha kiume kwa wakati tofauti. 
Kupitia katika wimbo wake uliobeba jina la album yake ijayo " Views From The 6" uliovuja hivi sasa, Drake ameonekana kuongelea wiki hizo mbili za mwishoni mwa February katika mashairi ya wimbo huo
You must remember wakin’ up in Paris with the blunt / You must remember f*ckin’ me like anytime you want/What made us wanna act like we were married for two weeks? / Now we back in California, we don’t even speak / That’s a no-no.


Katika wimbo huo Drake pia amesema "You make more money than i do, that sh*t attractive." Forbes iliripoti kwamba mwaka 2012 na 2013 ku ujumla Drake aliingiza mkwanja wa dola millioni 30 wakati Rihanna aliingiza dola millioni 48 kwa mwaka 2013 pake yake.
Wimbo huo pia umeshirikisha kipande cha sauti ya Rihanna kutokakwenye video ya youtube ambapo anasema "say hi M" baada ya Drake kuchana "with Jen and Melissa”. Melissa Forde ni rafiki wa karibu na Rihanna.