BONDIA Thomas Mashali 'Simba asiyefugika' anatarajia kupanda uringoni tena novemba 4 mwaka huu kumvaa mkenya Henry Wandera mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa New Madiba zamani Korini
Mashali anapigana uku akiwa na
historia ya kupoteza mpambano wake wa mwisho zidi ya bondia Mada Maugo
ambapo walicheza katika uwanja wa taifa na kupoteza kwa point mpambano
huo
akizungumzia mpambano huo Mashali
amesema atokubali kupoteza tena mchezo huuo ukizingatia anachezea
nyumbani kwao alopozaliwa na ndipo alipoanzia ngumi maeneo ya Tandale
hivyo sito kubali niaibike mbele ya ndugu zangu hivyo nawambia wapenzi
waje kwa wingi kuangalia mashali anavyofanya kazi yake ya mchezo wa
masumbwi
nae promota wa mpambano huo Khamis
Ally amewahakikishia kuwa sehemu ya parkingi ni kubwa na ulinzi ni wa
kutosha kifupi katika ulinzi tumejipanga vizuri pia siku hiyo kutakuwa
na mapambano mengine mazuri ya utangulizi ambapo mabondia wengi
wamejitokeza kucheza siku hiyo
siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa
mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa
mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama
Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na
wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi
Duniani
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni
mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio
mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi