FA CUP KUANZA NOVEMBA!! TANZANIA BARA


UWANJA_WA_TAIFA_DAR
MASHINDANO mapya Msimu huu, FA CUP, wenyewe TFF wanayaita Federation Cup, yanatarajiwa kuanza Mwezi Novemba Mwaka huu.
Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Timu zote zilizosajiliwa Nchini na ambazo zitaomba kushiriki na Droo yake haitabagua Timu za Madaraja tofauti katika upangaji Mechi zake za Mtoano.
Mechi za FA CUP zitachezwa katikati ya Wiki na Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa Msimu mpya wa 2014/15 imetambua hili kwa kupanga Mechi zake za Ligi Wikiendi tu.
Kwa mujibu wa habari toka TFF, Mashindano haya yatapewa msaada na FIFA na pia inatarajiwa Wadhamini mbalimbali wa ndani ya Nchi watashiriki kuyafadhili.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) itaanza Septemba 20 na kumalizika Tarehe 18 Aprili 2015.
LIGI KUU VODACOM
RATIBA-Mechi za Ufunguzi
Septemba 20
Azam FC v Polisi Moro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Yanga [Jamhuri, Morogoro]
Stand United v Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga]
Mgambo JKT v Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandizi]
Mbeya City v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]
Septemba 21
Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
MECHI ZA MOTO
DABI ya Kariakoo:
12-10-14 Yanga v Simba [Uwanja wa Taifa, Dar]
08-02-15 Simba v Yanga [Uwanja wa Taifa, Dar]
DABI ya Mbeya:
03-01-15 Mbeya City v Prisons [Sokoine, Mbeya]
11-04-15 Prisons v Mbeya City [Sokoine, Mbeya]
Mechi nyingine za Mvuto:
21-09-14  Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar]
09-11-14 Yanga v Azam FC [Uwanja wa Taifa, Dar]
20-12-14 Coastal Union v Yanga [Mkwakwani, Tanga]
01-01-15 Azam FC v Simba [Uwanja wa Taifa, Dar]
17-01-15 Coastal Union v Simba [Mkwakwani, Tanga]
TBA        Azam FC v Yanga [Uwanja wa Taifa, Dar]
28-03-15 Yanga v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar]
12-04- Simba v 15 Azam FC [Uwanja wa Taifa, Dar]