KAGAWA ARUDI DORTMUND T3NA, CHELSEA YAMNASA LOIC R EMY!

KAGAWA_N_GILWAKATI hii Leo Kiungo wa Manchester United kutoka Japan Shinji Kagawa akirudi Klabu yake ya zamani Borussia Dortmund, Straika wa QPR kutoka France Loic Remy amesainiwa na Chelsea.

Kagawa amesaini Mkataba wa Miaka Minne kurudi tena Borussia Dortmund ambako alichezea kuanzia 2010 hadi 2012 na kujiunga na Man United kwa Dau la Pauni Milioni 12.

Lakini Ada ya Uhamisho wake kurejea Dortmund haikutajwa.
Akiwa na Man United, Kagawa alifunga Bao 6 katika Mechi 57 alizochezea lakini hakuwa na namba ya kudumu.


LOIC_REMY
Chini ya Meneja mpya Louis van Gaal Kagawa amecheza Mechi moja tu na ni ile ya Capital One Cup Wiki iliyopita ambayo walifungwa 4-0 na MK Dons.

Kuondoka kwa Kagawa kunafuatia Man United kuwasaini Angel Di Maria kutoka Real Madrid na Daley Blind wa Ajax wakiungana na wapya wengine Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo.

WAKATI huo huo, Chelsea imetangaza kumsaini Straika wa Queens Park Rangers kutoka France Loic Remy kwa Dau la Pauni Milioni 10.5.

Remy, mwenye Miaka 27, alitakiwa pia na Arsenal lakini mapema hii Leo Klabu hiyo ilijitoa na kuiachia njia Chelsea kumnasa.

Mapema kwenye Kipindi hiki cha Uhamisho Remy alikuwa ajiunge na Liverpool lakini Klabu hiyo ilidai alishindwa upimwaji Afya yake kitu ambacho kiliwashangaza sana QPR.