Liverpool Leo hii wameinyuka Tottenham Uwanjani kwao White Hart Lane
kwa Bao 3-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kujipoza machungu ya
kuchapwa Bao 3-1 Jumatatu iliyopita.
Hadi Mapumziko, Liverpool walikuwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 8 la Raheem Sterling.
Kipindi cha Pili, Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, aliifungia
Timu yake Bao la Pili kwa Penati iliyotolewa na Refa Phil Dowd baada ya
Joe Allen kuchezewa rafu na Eric Dier.
Bao la Tatu lilifungwa na Alberto Moreno kwenye Dakika ya 60.
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Dier, Kaboul, Vertonghen, Rose, Bentaleb, Capoue, Chadli, Eriksen, Lamela, Adebayor.
Akiba: Chiriches, Holtby, Townsend, Kane, Dembele, Friedel, Davies
Liverpool: Mignolet, Manquillo, Moreno, Lovren, Sakho, Gerrard, Allen, Henderson, Sterling, Sturridge, Balotelli
Akiba: Brad Jones, Jose Enrique, Toure, Lambert, Coutinho, Can, Markovic
RefA: Phil Dowd