MAN CITY YAFUNGWA NYUMBANI GOLI 1 NASTOKE CITY

Saturday, 30 August 2014 20:14
Print PDF
BPL-2014-15-LOGO-BESTMABINGWA wa England, Manchester City, Leo wamechapwa kwa Uwanja wa Etihad Bao 1-0 .

Bao la ushindi la Stoke limefungwa na Mchezaji wa zamani wa Man United, Mame Biram Diouf, katika Dakika ya 28 baada ya kukokota Mpira Mita 70 na kumzidi akili Kipa Joe Hart.

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Stoke dhidi ya City katika Mechi 12 za Ligi Kuu England Uwanjani Etihad na umekuja chini ya Meneja Mark Hughes ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United na pia Meneja wa zamani wa City.
VIKOSI:
Manchester City: Hart, Sagna, Kolarov, Fernando (Fernandinho - 38'), Kompany, Demichelis, Nasri (Jesús Navas - 63' ), Yaya Touré, Agüero, Jovetic (Dzeko - 63'), Silva 
Akiba: Zabaleta, Milner, Dzeko, Caballero, Jesús Navas, Clichy, Fernandinho

Stoke City: Begovic, Bardsley, Pieters, Whelan, Shawcross, Wilson, Walters (Odemwingie - 45'), N'Zonzi, Crouch, Diouf, Moses (Muniesa - 80')
Akiba: Huth, Muniesa, Odemwingie, Arnautovic, Adam, Krkic, Sørensen
Refa: Lee Mason