
James Foley
Rais Barack Obama wa Marekani
amesema mauaji ya mwandishi wa habari James Foley raia wa Marekani
aliyeuawa na wapiganaji wa kundi la Kiislam yameishtua dunia.
Kauli hiyo ya Rais Obama inakuja huku wazazi wa mwandishi huyo wakielezea kutoridhishwa kwao na hatua zinazochukuliwa na Marekani kutokana na mauaji ya mtoto wao.
Wazazi hao wamesema wakati mwingine waandishi wa habari huru hawathaminiwi katika aki zao hata pale wanapojitolea maisha yao kwa ujira mdogo.
chanzo; BBC