
Maripota wasio na mipaka nchini Libya wameelezea wasiwasi wao mkubwa juu ya kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya wanaharakati wa habari na vituo vya upashaji habari nchini humo.
Mkuu wa uchunguzi katika taasisi ya kiraia ya maripota wasio na mipaka yenye makao yake mjini Paris, Ufaransa, Virgin Dongles amesema kuwa, kunashuhudiwa hali ya ukandamizaji mkuwa dhidi ya vyombo vya habari nchini humo.
Aidha Dongles amesema kuwa kuwa, kwa muda sasa Libya imekuwa uwanja wa mshambulizi makubwa dhidi ya waandishi wa habari na vituo vingine vya upashaji habari kutokana na mashambulizi yasiyokoma ndani ya taifa hilo.
Amevitaka pia vyombo vya habari nchini Libya hususan katika kipindi hiki ambacho bado taifa hilo la kaskazini mwa Afrika lingali linashuhudia mgogoro wa kisiasa na kiutawala, kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na bila ya upendeleo.
Kwengineko mkuu huyo wa idara ya uchunguzi katika taasisi ya kiraia ya maripota wasio na mipaka Virgin Dongles ameitaka serikali ya Tripoli kuchukua hatua za dharura kuwalinda maripota, waandishi wa habri na ofisi zao kutokana na kushambuliwa.