
Huo ni ushindi wa pili kwa Cameroon wakati Ivory Coast wameshinda moja na kufungwa moja.
Toka Kundi A, baada ya kuichapa Ugenini Nigeria Bao 3-2, Leo Congo wakiwa Nyumbani wameifunga Sudan Bao 2-0 ambao hicho ni kipigo chao cha pili baada kufungwa 3-0 wakiwa kwao Khartoum na South Africa Ijumaa iliyopita.
Nao Malawi, wakiwa Kundi B, wakiwa Nyumbani wamezinduka baada kupigwa 2-0 Ugenini na Mali kwa kuichapa Ethiopia 3-2.
Huko Stade de Kegue, Jijini Lome ilikuwa patashika wakati Wenyeji Togo, waliofungwa 2-1 Mechi ya kwanza na Guinea, walipoivaa Ghana iliyotoka Sare 1-1 na Uganda katika Mechi za Kundi E.
Togo walitangulia kupata Bao Dakika ya 12 Mfungaji akiwa Jonathan Ayite na Ghana kusawazisha Dakika ya 24 kwa Bao la Asamoah Gyan na Dakika ya 34 Emmanuel Agyemang-Badu kuipa Ghana Bao la Pili.
Togo walisawazisha Dakika ya 77 Mfungaji akiwa Emmanuel Adebayor lakini wakasonga mbele kwa Bao 3-2 kwa Bao la Dakika ya 85 la Atsu.
Huko Kampala, Uganda iliichapa Guinea 2-0 kwa Bao za Geofrey Massa.