BAYERN MUNICH YATOA SARE, DORTMUND YAFUNGWA

Hamburg v Bayern MunichMabingwa Watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich, Leo hii wametoka Sare ya 0-0 Ugeninikijuzi.blogspot.com na Hamburger SV lakini Vigogo wenzao, Borussia Dortmund, pia wakicheza Ugenini, walipigwa Bao 2-0 na FSV Mainz.

Mainz walipata Bao la kwanza katika Dakika ya 66 Mfungaji akiwa Shinji Okazaki.
Dakika ya 70 Shuti la Ciro Immobile lilizuiwa kwa mkono na Shinji Okazaki na Dortmund kupewa Penati iliyopigwa na Immobile lakini Kipa wa Mainz, Loris Karius, akaokoa.
Fußball Bundesliga 4. Spieltag 1. FSV Mainz - Borussia Dortmund
Dakika ya 74, Dortmund wakajifunga wenyewe baada Matthias Ginter kushindwa kuokoa na kutumbukiza Mpira wavuni na kuwafanya Mainz waongoze 2-0.

BUNDESLIGA
MATOKEO:

Jumamosi Septemba 20
Hamburger SV 0 Bayern Munich 0
Schalke 2 Eintracht Frankfurt 2
VfB Stuttgart 0 TSG Hoffenheim 2
FC Augsburg 4 SV Werder Bremen 2
SC Paderborn 2 Hannover 0
FSV Mainz 2 BV Borussia Dortmund 0