CHELESEA YAJIIMARISHA KILELENI COSTA APIGA HATRICK, REMY NAE ACHANA NYAVU

Diego Costa ashanglia moja magoli yake,amefunga magoli matatu (hat trick)  
MSHAMBULIAJI Diego Costa ameendeleza mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifungia Cheslea mabao matatu peke yake katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Swansea City Uwanja wa Stamford Bridge, London.

Wakati mchezaji huyo bora wa Agosti, akipiga hat trick yake ya kwanza England na kufikisha mabao saba ndani ya mechi nne, bao lingine la Chelsea lilifungwa na mchezaji mpya, Loic Remy aliyeingia kuchukua nafasi ya Coasta kipindi cha pili.

 Beki John Terry alijifunga kuipatia Swansea ambayo bao lake lingine lilifungwa na Jonjo Shelvey.

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas/Salah dk82, Schurrle/Ramires dk46, Oscar, Hazard na Diego Costa/Remy dk72.
Swansea: Fabianski, Rangel, Amat/Fernandez dk46, Williams, Taylor, Ki, Shelvey, Sigurdsson, Dyer, Routledge/Montero dk66 na Gomis/Bony dk76.

MATOKEO MENGINE
CRYSTAL PALACE 0 BURNLEY 0
Kipa wa Crystal Palace Julian Speroni  aliokoa Penati ambayo iliwapa Sare ya 0-0 na Burnley.
Penati hiyo ilipigwa Dakika ya 85 na Scott Arfield.
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Ward, Delaney, Dann, Mariappa, Jedinak (c), McArthur, Puncheon, Zaha, Campbell, Gayle.
Akiba: Hennessey, Fryers, Kelly, Ledley, Williams, Ledley, Bolasie, Doyle.
Burnley: Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Arfield, Marney, Jones, Boyd, Jutkiewicz, Ings.
Akiba: Gilks, Reid, Ward, Wallace, Sordell, Long, Barnes.
REFA: Mike Dean

SOUTHAMPTON 4 NEWCASTLE 0
Bao mbili za Straika wa Italy Graziano Pelle, moja la Jack Cork na Schneiderlin zimewapa ushindi wa Nyumbani Southampton walipoitandika Newcastle Bao 4-0.
VIKOSI:
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Alderweireld, Bertrand, Cork, Schneiderlin, S. Davis, Tadic, Long, Pellè.
Akiba: K. Davis, Yoshida, Gardos, Wanyama, Ward-Prowse, Mayuka, McQueen.
Newcastle: Krul; Janmaat, Coloccini, Williamson, Haidara; Colback, Anita; Cabella, Sissoko, Gouffran; Riviere.
Akiba: Elliot, S.Taylor, Tiote, Obertan, Ameobi, Armstrong, Perez.
REFA: Chris Foy

STOKE 0 LEICESTER 1
Bao la Dakika ya 64 la Leonardo Ulloa limewapa Leicester City, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu, ushindi wa Ugenini wa Bao 1-0 dhidi ya Stoke City.
VIKOSI:
Stoke: Begovic; Bardsley, Shawcross, Wilson, Pieters; Whelan, Nzonzi; Moses, Bojan, Walters; Crouch.
Akiba: Sorensen, Huth Muniesa, Arnautovic, Adam, Diouf, Assaidi.
Leicester: Hamer, De Laet, Morgan, Moore, Konchesky, Mahrez, Hammond, King, Schlupp, Ulloa, Nugent.
Akiba: Smith, Drinkwater, Vardy, Cambiasso, Knockaert, Wasilewski, Wood.
REFA: Michael Oliver

SUNDERLAND 2 TOTTENHAM 2
Hii Mechi ilianza kwa moto kwani Tottenham walipata Bao katika Dakika ya Pili tu baada ya Shuti la Emmanuel Adebaypr kutemwa na Kipa Mannone na Nacer Chadli kufunga lakini Dakika mbili baadae, Adam Johnson aliwatoka Mabeki wawili na kupinda Shuti murua na kuipa Sunderland Bao la kusawazisha.
Kipindi cha Pili Christian Eriksen aliipa Spurs Bao la Pili na Sunderland walisawazisha kwa Bao la kujifunga wenyewe Spurs kupitia Harry Kane.
VIKOSI:
Sunderland: Mannone, Vergini, van Aanholt, Brown, O’Shea, Cattermole, Larsson, Rodwell, Johnson, Alvarez, Wickham.
Akiba: Pantilimon, Jones, Bridcutt, Gomez, Giaccherini, Buckley, Altidore
Tottenham: Lloris, Dier, Kaboul, Chiriches, Rose; Dembele, Capoue; Lamela, Eriksen, Chadli; Adebayor.
Akiba: Vorm, Fazio, Naughton, Lennon, Stambouli, Townsend, Kane.
REFA: Craig Pawson

WEST BROM 2 EVERTON 0
Bao la Dakika ya Pili la Romelu Lukaku na la Kipindi cha Pili la Kevin Mirallas yamewapa ushindi wa Ugenini Everton walipoichapa West Bromwich Albion Bao 2-0.
VIKOSI:
West Bromwich Albion: Foster, Wisdom, Olsson, Dawson, Pocognoli, Morrison, Gardner, Brunt, Dorrans, Berahino, Ideye.
Akiba: Daniels, Gamboa, Baird, Yacob, McAuley, Blanco, Samaras.
Everton: Howard, Coleman, Baines, Jagielka, Stones, Barry, McCarthy, Mirallas, Naismith, McGeady, Lukaku.

Akiba: Robles, Alcaraz, Garbutt, Gibson, Besic, Osman, Atsu.
REFA: Anthony Taylor