EURO2016;GERMANY YASHINDA MULLLER ATUPIA 2, URENO HOI BILA RONALDO

MABINGWA DUNIANI, Germany, wakicheza Mechi yao ya kwanza ya Mashindano rasmi tangu wachukue Kombe la Dunia hapo Julai 13 kwa kuichapa Argentina Bao 1-0, Jana Usiku kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi D la EURO 2016 na Scotland walishinda 2-1.

Germany walifunga Bao katika Dakika ya 18 kwa Kichwa cha Thomas Muller na Ikechi Anya kuisawazishia Scotland Dakika ya 66 baada ya kazi njema ya Nahodha Darren Fletcher.

Lakini Dakika 4 baadae Thomas Muller akawapa Germany Bao la Pili baada kuunasa Mpira wa Kona.

VIKOSI:
Germany: Neuer, Rudy, Boateng, Höwedes, Durm; Kramer, Kroos; Müller, Reus, Schürrle; Götze.
Akiba: Zieler, Weidenfeller, Ginter, Rüdiger, Grosskreutz, Sam, Podolski.

Scotland: Marshall, Hutton, Whittaker, R.Martin, Hanley; Morrison, D.Fletcher, Mulgrew, Bannan, Anya; Naismith.
Akiba: A. McGregor, Greer, Maloney, S.Fletcher, Bryson, McDonald, Burke, Reynolds, McArthur, Gordon, Forsyth, C.Martin.


PORTUGAL 0 ALBANIA 1
WAKICHEZA bila ya Nahodha wao ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, na Timu kucheza chini ya uongozi wa Winga wa Manchester United, Nani, ambae yuko Portugal kwa Mkopo Klabuni Sporting Lisbon, Portugal walianza Mechi yao ya kwanza ya Kundi I kwa kufungwa Nyumbani kwao na Albania Bao 1-0.

Albania walipata Bao lao la uhindi Dakika ya 52 Mfungaji akiwa Bekim Balaj kufuatia kuzubaa kwa Difensi ya Portugal
VIKOSI:
PORTUGAL: Rui Patricio; Joao Pereira, Pepe, Ricardo Costa, Coentrao; Andre Gomes, W.Carvalho, Moutinho; Vieirinha, Eder, Nan

ALBANIA: Berisha; Hysaj, Cana, Mavraj, Agolli; Roshi, Xhaka, Kukeli, Abrashi, Lenjani; Balaj.

EURO 2016
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Septemba 7
Denmark 2 Armenia 1 [Kundi I]
Hungary 1 Northern Ireland 2 [Kundi F]
Georgia 1 Ireland 2 [Kundi D]
Germany 2 Scotland [Kundi D]
Faroe Islands 1 Finland 3 [Kundi F]
Greece 0 Romania 1 [Kundi F]
Portugal 0 Albania 1 [Kundi I]
Gibraltar 0 Poland 7 [Kundi D]

Jumatatu Septemba 8
19:00 Russia v Liechtenstein [Kundi G]
21:45 Luxembourg v Belarus [Kundi C]
21:45 Austria v Sweden [Kundi G]
21:45 San Marino v Lithuania [Kundi E]
21:45 Spain v Macedonia [Kundi C]
21:45 Estonia v Slovenia [Kundi E]
21:45 Switzerland v England [Kundi E]
21:45 Ukraine v Slovakia [Kundi C]
21:45 Montenegro v Moldova [Kundi G]

Jumanne Septemba 9
19:00 Kazakhstan v Latvia [Kundi A]
19:00 Azerbaijan v Bulgaria [Kundi H]
21:45 Croatia v Norway [Kundi H]
21:45 Norway v Italy [Kundi H]
21:45 Czech Republic v Netherlands [Kundi A]
21:45 Iceland v Turkey [Kundi A]
21:45 Andorra v Wales [Kundi B]
21:45 Bosnia/Herzegovina v Cyprus [Kundi B]
21:45 Israel v Belgium [Kundi B]