Ukiskia wimbo Diamond amechana badala ya kuimba, lazima utataka kuusikia
wimbo huo umekaa vipi sio? sasa wimbo huo ndio huu "Mototo Wa Mama"
ulio chini ya project ya mdogo wa producer Macochali "Zachaa"
Zachaa amedai kutengeneza project hiyo ambayo mpaka hivi sasa
imekamilisha nyimbo 7 kwa sababu ya kujiingizia kipato, maana wasanii
anaofanya nao kazi huwa wanalipa tu hela ya studio na kumuacha akiwa
hana haki zingine zinazotokana na kazi hiyo kama ringtones na zinginezo,
huku akitolea mfano wa wimbo wa Madee "Pombe yangu" ambao aliufanya
yeye na kumbadilisha Madee kutoka kuchana mpaka aina ya muziki
anaoufanya sasa hivi.