
kijuzi.blogspot.comSoko la hisa la DSM- DSE- limefunga wiki, kwa mauzo manono ya zaidi ya shilingi BILIONI MOJA NUKTA MOJA. Hisa za benki za biashara za CRDB, DCB na NMB zikiwa zinaongoza kwa kupata wawekezaji wengi wapya.
Tathmini ya mwenendo wa biashara wa soko hilo imeonesha kuwa hisa zipatazo LAKI TATU zimeuzwa katika soko la leo katika mikupuo 62.
Hisa nyingine zilizofanya vizuri ni za kampuni za saruji za SIMBA na TWIGA pamoja na hisa za kampuni ya kuzalisha gesi ya viwandani ya --TOL ambazo zimeuzwa kwa bei moja tu ya shilingi 480 kwa hisa katika mikupuo miwili.