JUKWAA LA WAHARIRI LALAANI KITENDO CHA POLISI KUWAPIGA WAANDISHI WA HABARIAA

Mwenyekiti wa TEF ABSALOM KIBANDA
Jukwaa la wahariri nchini TEF limeelani na kueleza kusikitishwa kwake na kitendo cha polisi kuwapiga waandishi wa habari watatu waliokuwa katika majukumu yao ya kuhabarisha umma katika eneo la Makao Makuu ya Polisi jijini DSM katika tukio la Mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE kwenda kuhojiwa na POLISI.

Mwenyekiti wa TEF ABSALOM KIBANDA, amesema ni vigumu kuamini kwamba askari waliotekeleza kitendo hicho walifanya hivyo kwa bahati mbaya kwa vile waandishi hao walijitambulisha kwa kutumia vitambulisho vyao vya kazi kabla ya tukio hilo.

Jukwaa la Wahariri limetaka jeshi la polisi kama taasisi kuthibitisha kutoshiriki kwake katika vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari kwa kuchukua hatua za wazi dhidi ya askari walioshiriki katika mashambulizi dhidi ya wanahabari 

Akizungumzia kitendo hicho, Msemaji wa Jeshi la polisi nchini ADVERA BULIMBA amesema jeshi hilo litatao tamko lake baadaye. 
kijuzi.blogspot.com
Waandishi waliopigwa na polisi ni YUSUF BADI wa TSN, JOSEPAHAT ISANGO wa Free Media na SHAMIM AUSI wa Gazeti HOJA.