WACHEZAJI wa Borussia Dortmund, Ilkay Gündogan na Shinji Kagawa, wamevaa Jezi Nyeusi na Njano kwa mara ya kwanza Msimu huu wakati Timu yao ilipocheza na Kikosi cha Vijana wao wa chini ya Miaka 23 kwenye Mechi ya kujipima hapo Ijumaa.
Wakati Kagawa ndio kwanza amehamia Dortmund kutoka Manchester United, Gundogan alikuwa Majeruhi wa muda mrefu baada ya kuumia Mgongo kwenye Mechi ya kwanza tu ya Msimu uliopita wa 2013/14.
Kagawa alionekana kama hakuwa ameondoka Timu hiyo aliyoichezea kati ya 2010 na 2012 kabla kwenda Man United kwani alikifungia Kikosi cha Kwanza cha Dortmunda Bao la Kwanza katika Dakika ya 13 tu.
Mpaka mwisho wa Mechi hiyo, Kikosi cha Kwanza kiliifunga U-23 Bao 3-1.



