Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba imewasilisha rasimu ya katiba inayopendekezwa mbele ya Wajumbe wa bunge hilo Mjini DODOMA.
Akiwasilisha rasimu hiyo ya katiba inayopendekezwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya bunge hilo ANDREW CHENGE ametaja mambo kadhaa yaliyozingatiwa na kuiongoza kamati hiyo wakati wa kuandaa rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
CHENGE pia akaeleza yale yanayopendekezwa katika sura ya Nane ya Rasimu hiyo ya Katiba inayopendekezwa ambayo pamoja na mambo mengine inahusu masuala ya uongozi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kazi ya uandaaji ya rasimu hiyo ya katiba inayopendekezwa imefanywa na Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba kwa kuzingatia maoni ya Kamati zote Kumi na Mbili za Bunge Maalum la Katiba.