KAMBI YA UPINZANI KENYA YAITAKA SERIKALI KUKOMA KUTOA VITISHO KWA MAGAVANA


Upinzani Kenya: Serikali ikome kuwatishia magavanaKambi ya upinzani nchini Kenya imeitaka serikali kukoma kutoa vitisho kwa magavana wasiokubaliana na jinsi ikulu ya Nairobi inavyoendesha mambo.

 Kiongozi wa muungano wa upinzani wa CORD, Raila Odinga, amemwambia Rais Uhuru Kenyatta kwamba, matamshi yake ya vitisho dhidi ya magavana wanaopinga utendakazi wa serikali ni kinyume cha sheria.

 Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita Rais Kenyatta aliwaonya magavana kutoka muungano  unaotawala wa Jubilee akisema wale watakaoendelea kupigia chapuo kufanyika kura ya maamuzi kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo watavuliwa uanachama ili watafute kura upya kama watu binafsi. 

Magavana wanataka kura ya maamuzi ifanyike ili serikali kuu ishurutishwe kutoa fedha zaidi kwa ajili ya maendeleo ya kaunti.

 Takwa la magavana linawiana na lile la upinzani kuhusu kura ya maamuzi ingawa malengo ya pande mbili hizo yanatofautiana.