![]() |
katibu mkuu wa CCM ABDULRAHMAN KINANA |
kijuzi.blogspot.comKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ABDULRAHMAN KINANA amewaonya Viongozi wa serikali za Vijiji na Mitaa nchini kuacha mara moja vitendo vya uuzwaji wa ardhi tofauti na kiwango walichopangiwa kisheria.
KINANA ametoa onyo hilo baada ya kukithiri vitendo vya uuzwaji wa ardhi kuanzia Hekta 2,000 na kuendelea tofauti na sheria inayowataka wauze kiwango cha ardhi cha ekari 50 tu.
KINANA anaendelea na ziara yake mkoani Pwani na kwasasa yupo wilayani Kisarawe, ambapo pamoja na mambo mengine ameshiriki shughuli za ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti Monchware katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe.