Mafuriko mapya yamelikumba eneo la kaskazini mashariki mwa INDIA na kusababisha vifo vya watu 43.
Mafuriko hayo yanaambatana na maporomiko ya udongo na vijiji vipatavyo 90 vimeathiriwa na mafurika hayo mapya.
Maeneo mengine nchini INDIA bado yako chepechepe, baada ya nchi hiyo kukumbwa na mafuriko mengine katika siku za hivi karibuni.
Maelfu ya wafanyakazi wa vikosi vya misaada wamekwenda katika eneo la tukio kujaribu kuwaokoa watu ambao bado wamekwama katika nyumba zao.
kijuzi.blogspot.com
Zaidi ya watu laki moja katika maeneo mbalimbali nchini INDIA wameamriwa kuyahama makazi yao na kuhamia katika maeneo yenye miinuko.
Zaidi ya watu laki moja katika maeneo mbalimbali nchini INDIA wameamriwa kuyahama makazi yao na kuhamia katika maeneo yenye miinuko.