MANCHESTER UNITED YAANZA LIGI RASMI

Manchester United Leo wameshinda Mechi yao ya kwanza Msimu huu kwenye Ligi Kuu England wakati Kikosi chao kipya kikiisambaratisha QPR kwa Bao 4-0 ndani ya Old Trafford huku Angel De Maria aking’ara na Wachezaji wapya Marcos Rojo na Daley Blind wakicheza Mechi yao ya kwanza na kuleta uhai mkubwa.
ANGELDIMARIA-AKIMTESA-SANDRO-QPR
Bao 3 kabla ya Mapumziko, zilizofungwa na Di Maria, Ander Herrera na Wayne Rooney ziliwaua QPR na kuwamaliza kabisa pale Kipindi cha Pili Juan Mata alipofunga Bao la 4.
Straika mpya, Radamel Falcao, alikuwa Benchi na kuingizwa Dakika ya 67 na alionyesha matumaini na nusura afunge Bao kama si uhodari wa Kipa wa Robert Green.

MAGOLI:
Angel Di Maria Dakika ya 24
Aguera Ander Herrera 36
Wayne Rooney 44
Juan Mata 58

Angel Di Maria alifunga Bao la Kwanza kwa frikiki murua na ni yeye alietengeneza Bao la Pili kwa kukokota ngoma Mita 60 na kumpasia Rooney aliepiga Shuti lililookolewa na kumrudia Herrera na kufunga.

DONDOO MUHIMU:
-Bao la Wayne Rooney hii Leo ni Bao lake la 175 akifungana na Thierry Henry kwa Wafungaji Bora katika Historia ya Ligi Kuu England.
-Nambari Wani Mfungaji Bora Ligi Kuu England ni Alan Shearer, Bao 260 na wa Pili ni Andy Cole, Bao 189.

Rooney alifunga Bao la 3 kabla ya Haftaimu baada ya ushirikiano mzuri wa Mata, Herrera na mwenyewe Rooney.
Bao la 4 lilifungwa na Juan Mata baada kuunganisha Mpira wa Di Maria.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumapili ijayo Ugenini kucheza na Leicester City.
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea, Rafael, Evans, Rojo, Blackett, Blind, Herrera, Mata, Di Maria, Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Shaw, Fletcher, Januzaj, Valencia, A Pereira, Falcao.

QPR: GreenCaulkerAustinPhillipsFerdinandHillIslaSandroFerHoilettKranjcar
Akiba: Traore, McCarthy, Onuoha, Henry, Vargas, Zamora, Taarabt