MECHI ZA KIRAFIKI: FRANCE YAIPIGA SPAIN, ITALY YAIUA MTU 10 HOLLAND!

>>DE GEA AANZA LAKINI SPAIN YATUNGULIWA!
FRANCE-REMY-AFUNGAKATIKA Mechi za Kimataifa za Kirafiki zilizochezwa Usiku huu, Guus Hiddink alikumbana na kipigo katika Mechi yake ya kwanza kama Kocha wa Holland na kumpa kicheko mpya mwenzake Antonio Conte wa Italy wakati France ikiwatungua Spain.

SOMA ZAIDI:
ITALY 2 HOLLAND 0
Ndani ya Stadio San Nicola huko Bari, Meneja mpya wa Italy Antonio Conte alipambana na Meneja mpya wa Holland Guus Hiddink na kuibuka kidedea baada ya Italy kuichapa Holland Bao 2-0.


Bao zote za Italy zilifungwa ndani ya Dakika 10 za kwanza ambazo pia zilishuhudia Holland wakibakishwa Mtu 10 baada ya Bruno Martins Indi kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Italy walicheza Mechi hii huku wakiwa na Mastraika Ciro Immobile na Simone Zaza aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza kwa Nchi yake.

Iliwachukua Dakika 3 tu kwa Italy kufunga Bao la kwanza kupitia Ciro Immobile aliepokea pasi ndefu toka kwa Leonardo Bonucci na kumpita Kipa Jasper Cillessen na kufunga.

Bao la Pili la Italy lilifungwa kwa Penati ya Daniele de Rossi ya Dakika ya 10 ambayo ilitokana na Rafu kwa Simone Zaza aliyofanya Bruno Martins Indi alietolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

VIKOSI:
ITALY: Sirigu; Ranocchia, Bonucci, Astori; Darmian, Marchisio, De Rossi, Giaccherini, De Sciglio; Immobile, Zaza
Akiba: Buffon, Padelli, Perin, Ogbonna, Candreva, Florenzi, Maggio, Parolo, Pasqual, Verratti, Destro, Giovinco, Quagliarella, Poli, Chiellini, El Shaarawy

HOLLAND: Cillessen; Janmaat, De Vrij, Martins Indi, Blind; Wijnaldum, De Jong, Sneijder; Kuyt, Van Persie, Lens
Akiba: Van Der Wiel, Van Dijk, Veltman, Pieters, Verhaegh, Narsingh, Afellay, Fer, Klassen, Depay, Krul, Zoet

FRANCE 1 SPAIN 0
Zikiwa zimebaki Dakika 16, ushirikiano mzuri wa Sissoko na Valbuena ulimfungulia Loic Remy kufunga Bao 1 na la ushindi wakati France wanaichapa Spain Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa Stade de France Jijini Paris.

VIKOSI:
FRANCE: Lloris, Debuchy, Varane, Sakho, Evra, Pogba, Matuidi, Sissoko, Valbuena, Griezmann, Benzema
Akiba: S. Mandanda, S. Ruffier, B. Sagna, J. Mathieu, L. Digne, E. Mangala, M. Schneiderlin, R. Mavuba, R. Cabella, Y. Cabaye, A. Lacazette, L. Rémy

SPAIN: De Gea, Carvajal, Ramos, San Jose, Azpilicueta, Busquets, Cazorla, Koke, Raul Garcia, Fabregas, Costa
Akiba: Kiko Casilla, Casillas, Jordi Alba, Juanfran, Albiol, Bartra, Iturraspe, David Silva, Isco, Paco Alcácer, Pedro

MECHI ZA KIMATAIFA ZA IRAFIKI
RATIBA/MATOKEO:
Alhamisi Septemba 4
**Saa za Bongo
Slovakia 1 Malta 0
Sweden 2 Estonia 0
Bosnia-Herzegona 3 Liechtenstein 0
Croatia 2 Cyprus 0
Belgium 2 Australia 0
Italy 2 Netherlands 0
France 1 Spain 0

Ijumaa Septemba 5
1345 Japan v Uruguay

Jumamosi Septemba 6
0400 Brazil v Colombia

Jumapili Septemba 7
0500 Chile v Mexico
2145 Serbia v France

Jumatatu Septemba 8
1400 South Korea v Uruguay
2300 Saudi Arabia v Australia

Jumatano Septemba 10
0300 Chile v Haiti
0500 Brazil v Ecuador
0500 Mexico v Bolivia