Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa BERNARD MEMBEkijuzi.blogspot.com
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa BERNARD MEMBE amesema nchi zote duniani ikiwemo Tanzania zinawajibu wa kufanyia kazi kwa umakini vitisho vya usalama wa dunia na watu wake kama alivyoelekeza Rais BARACK OBAMA wa MAREKANI alipokua akifungua rasmi Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika Mjini NEW YORK nchini MAREKANI.
MEMBE pamoja na viongozi wengine waandamizi walioambatana na Rais JAKAYA KIKWETE kuiwakilisha Tanzania Katika Mkutano huo, wamempongeza Rais BARACK OBAMA kwa kutangaza kuwa nchi yake ipo tayari kushirikiana na mataifa mengine duniani kukabiliana na vitisho vya usalama.
Miongoni mwa vitisho hivyo ni pamoja na Ugaidi, makundi ya imani kali, wapiganaji wanaoendesha mauaji dhidi ya raia wasio na hatia pamoja na kukabiliana mabadiliko ya tabia nchi.
