
Maher Abu Sabha amesema tangu mwaka 2006 hadi sasa eneo la Gaza limeekewa mzingiro mkubwa na utawala wa Kizayuni wa Israel lakini tangu wakati huo hadi sasa Mahmoud Abbas hajachukua yoyote ya maana ili mzingiro huo uondolewe.
Kwa mujibu wa Abu Sabha uzembe uliofanywa na Rais huyo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika kadhia ya mzingiro wa Gaza inajenga dhana kwamba anashirikiana na Israel katika kuendeleza mzingiro huo.
Katika upande mwengine afisa mmoja mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema Misri imejiondoa katika usimamizi wa mazungumzo baina ya harakati hiyo na ile ya Fat-h.
Muhammad Nizal amesema kutokana na kujiondoa Misri kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo imekubaliwa kwamba kuanzia sasa mazungumzo baina ya harakati hizo za Palestina yatafanyika katika Ukanda wa Gaza.
Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri hadi sasa haijatoa taarifa rasmi kuhusiana na suala hilo