MOURINHO ASEMA UEFA IIADHIBU ZAIDI MAN CITY KWA KUVUNJA SHERIA

MOURINHO-CHELSEA_TRAININGJosé Mourinho amesema Klabu ambazo zinavunja Kanuni za FFP za UEFA, Manchester City miongoni mwao, zitaogopa kurudia kosa hilo ikiwa tu zitakatwa Pointi na si kupigwa Faini.

Man City walipigwa Faini ya Pauni Milioni 50 kwa kukiuka FFP, Financial Fair Play, inayotaka kila Klabu ijiendeshe kwa Mapato yake yenyewe na pia Kikosi chao cha UEFA CHAMPIONZ LIGI kupunguzwa kutoka Wachezaji 25 hadi 21.
Man City watalipa Faini ya Pauni Milioni 20 tu ikiwa katika Misimu ijayo hawatarekodi Hasara katika Mahesabu yao.

Pamoja na Man City, Klabu nyingine zilizoadhibiwa ni Paris Saint-Germain na Zenit St Petersburg lakini Chelsea imenusurika kwa kutii FFP na Mtendaji wao Mkuu, Ron Gourlay, amekiri kuwa ilikuwa kazi ngumu kuilinda biashara yao na kutotegemea Fedha toka Mmiliki wao Roman Abramovich.

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ameipinga UEFA kwa kupiga Faini tu na kudai: “Kila Mtu anajua kuna Faini tu! Lakini hizi Faini ni haki? Sidhani. Kwa maoni yangu kitu cha kwanza kufanya ni Klabu hizo kukatwa Pointi na kuwaondolea Mataji yao. Kama una Fungu la Fedha ambalo linakuruhusu kukiuka FFP na unashinda Mataji na unapigwa Faini tu, utafanya kile kile tu!”

Jumapili Chelsea wanasafiri kwenda Jijini Manchester kucheza Uwanjani Etihad na Man City, Mabin
gwa wa England, katika Mechi kali ya Ligi Kuu England.
Mvuto mwingine kwa Mechi hii ni uwezekano wa aliekuwa Gwiji wa Chelsea, Frank Lampard, kuonekana akivaa Jezi ya City kuikabili Chelsea.

Lampard aliondoka Chelsea mwishoni mwa Msimu uliopita na kujiunga na Klabu mpya ya MLS, Major League Soccer, huko Marekani, New York City FC, ambayo itaanza Ligi Mwakani na Klabu hiyo, ambayo ni Mshirika wa City, kumkopesha Mchezaji huyo kuichezea City.

Lakini Mourinho amesema hali hii haimharibii Lampard kurudi baadae Chelsea kufanya kazi nyingine.

Mourinho amesema: “Hili halijaharibu lolote. Anaweza kurudi Chelsea wakati wowote akitaka na hiyo ni kauli ya Abramovich!”

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Manchester City:
Hart, Zabaleta, Kompany, Demichellis, Kolarov, Navas, Toure, Fernandinho, Silva, Aguero, Dzeko
Akiba:  Nastasic, Boyata, Milner, Caballero, Wright, Sinclair, Sagna, Lampard, Clichy, Mangala, Nasri

Chelsea:
Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Fabregas, Matic, Schurrle, Costa, Hazard
Akiba: Cech, Schwarzer, Filipe Luis, Ake, Christensen, Zouma, Baker, Oscar, Mikel, Willian, Salah, Drogba, Rémy

REFA: Mike Dean