kijuzi.blogspot.com
Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli amefunga bao lake la kwanza leo Liverpool dakika ya 81, akiwasawazishia Wekundu hao baada ya Dani Abalo kutangulia kuifungia Ludogorets.
Nahodha Steven Gerrard aliihakikishia Liverpool kushinda mechi ya kwanza ya makundi kwa bao la penalti dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Lovren, Sakho, Moreno, Henderson, Gerrard, Lallana/Borini dk67, Sterling, Coutinho/Lucas dk67 na Balotelli.
Ludogorets: Borjan, Caicara, Moti, A Aleksandrov, Minev, Dyakov, Abel, M Aleksandrov, Marcelinho, Misidjan na Bezjak.

Mario Balotelli akishangilia baada ya kuifungia Liverpool
