NDANDA FC YAANZA LIGI KILELENI KWA USHINDI WA 4-1


Ndanda FC imeonyesha imepania kufanya kweli, imeichapa Stand United kwa mabao 4-1.

Ikiwa ndiyo mechi ya kwanza kwa timu hizo ya Ligi Kuu Bara, Stand ikiwa nyumbani Kambarage imelala kwa mabao hayo 4-1.
Wageni Ndanda walipata mabao yao kupitia Paul Ngalema, Nassor Kapama na  Ernest Mwalupani.
Wakati wenyeji ambao walijitahidi kurekebisha mambo walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Salum Kamana.

Mechi ilikuwa nzuri nay a kuvutia lakini wageni ndiyo walioonyesha soka la kuvutia zaidi.kijuzi.blogspot.com