Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri.
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul 'Diamond Platnumz'
alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini
Stuttgart,
Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio
waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijikuta
wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki
Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Mr.Awin Williams Akipomiemie
raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki hao walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza
kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.
Kilichowakera zaidi mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa
katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja vyombo vya
muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo hosptalini kwa sasa.
Moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa
mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ
Drazee naye yupo hoi hospatal.
Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hilo la aibu halijawahi kutokea,
kwani msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari
sana kwani mashabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia
itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia
anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Hivi ndivyo ukumbi huo ulivyokuwqa baada ya tafrani hiyo.