Aliekuwa msanii wa nyimbo za bongo fleva "QJay" na kuamua kuachana na
mziki huo kwa kuwa ameamua kumrudia mungu "ameokoka" anamba sapoti yako
kwa kazi anayoifanya hivi sasa.
QJay ambae kwa sasa anafanya kazi aliyokuwa akiifanya mwanzo kabla ya
kuanza muziki ambayo ni kutengeneza vifaa vinavyohusisha chuma kama
vitanda, mageti na madirisha anaomba sapoti yenu kwa kununua kazi zake
kwa dizaini yoyote unayoitaka na anapatikana maeneo ya Mbezi Makonde
"ndio ujuzi ambao nilikuwa nao kabla sijafahamika katika music, ndio
kazi ambayo naifanya, kwahiyo kama kuna watu wanahitaji vitu vya namna
hiyo vya chuma kwa mfano mageti, madirisha vitanda any disgn ambayo
inahusika na chuma wanaweza wakaniona, niko maeneo ya mbezi makonde kama
unashuka barabara ya kwenda NSSF, karibu na nyumba za NSSF maeneo ya
mkonde makonde chini kule" amesema
QJay pia amedai kutokuhitaji loyalty yoyote ile inayotokana na kazi za
muziki aliowahi kuufanya mwanzo ikiwa ni pamoja na ringtones na kuwa
muziki wa gospal ataufanya pale tu atakapo kuwa na uelewa mzuri wa dini
yake na mambo yanayoizunguka dini yake ila kwasasa amerudia kazi yake
hiyo ya mwanzo
Chanzo; DJ Fety