Home
About
Contact
Home
KITAIFA
KIMATAIFA
MICHEZO
BUIRUDANI
MAKALA
Home
MICHEZO
SAMATA NA ULIMWENGU KUIBEBA TP MAZEMBE LEO?
SAMATA NA ULIMWENGU KUIBEBA TP MAZEMBE LEO?
kijuzi
Saturday, September 20, 2014
KLABU ya Entente Setif ya Algeria insingia kwenye mechi ya kisasi dhidi ya TP Mazembe katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Stade du 8 Mai 1945 usiku wa leo.
Huo utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo mfululizo kwa michuano ya Afrika, baada ya awali kukutana mwaka jana katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Mazembe haikufungwa na Setif katika Kundi B wakitoa safe ya 1-1 nchini Algeria kabla ya kuwafunga 4-2 mjini Lubumbashi.
Mbwana Samatta anatarajiwa kuendelea kuibeba Mazembe leo
Setif ilishika mkia katika Kundi B wakati Mazembe ilikwenda Nusu Fainali ambako walitolewa na CS Sfaxien ya Tunisia kwenye fainali kwa kufungwa 1-0 matokeo ya jumla.
kijuzi.blogspot.com
“Tutajaribu kulipa kisasi cha kufungwa 4-2 msimu uliopita, na pia tulikutana nap katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2010,” alisema kocha wa Setif, Kheireddine Madoui.
Setif haijafungwa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu chini ya kocha mwenye umri wa miaka 37 na ilitinga Nusu Fainali baada ya sare nne na kushinda mechi mbili kwenye kundi lake.
Wakati huo huo, Mazembe haina rekodi ya uhakika ya mechi za ugenini, imefungwa mara mbili na kutoa sare tatu katika mechi zake tano za ugenini mwaka huu.
Lakini kiungo Rainford Kalaba, anaamini wanaweza kushinda mechi yao ya kwanza ugenini leo tangu Machi, 2013 walipoichapa Centre Chiefs of Botswana 1-0.
"Moyoni mwangu, naweza kufikiria kitu hicho tu: Kwenda Setif kushinda. Mechi za Nusu Fainali zina uzito tofauti, kwa sababu zinafungua milango ya fainali," amesema Kalaba.
Washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanatarajiwa kuendelea kuibeba Mazembe leo.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya AS Vita ya DRC dhidi ya CX Sfaxien ya Tunisia mjini Kinshasa.
Popular Posts
RANGI YA MWAKA 2018 NI PURPLE (UTRA VIOLET PURPLE 18-3838)
Friday, December 29, 2017
MAREKANI YAINYOOSHEA CHINA KIDOLE DHIDI YA KUKIUKA VIKWAZO VYA UN KWA KOREA KASKAZINI
Friday, December 29, 2017
MAHAKAMA KUU YAMUACHIA HURU SHEIKH PONDA
Tuesday, December 19, 2017
VIDEO ZA PICHA ZA UTUPU ZA ZARI ZAVUJA MTANDAONI
Saturday, December 06, 2014
RANGI YA MWAKA 2017 INAITWA "GREENERY"
Wednesday, June 07, 2017
MZEE AHOFIA KABURI LAKE KUUZWA
Saturday, December 06, 2014
A-Z ZILE SAUTI ZA KIMAHABA KATI YA MBOWE NA WEMA MTANDAONI MCHEZO MZIMA HUU HAPA
Tuesday, June 13, 2017
LILY WAYNE ATISHIA KUONDOKA YMCMB KISA KUZUIWA ALBAMU YAKE
Saturday, December 06, 2014
WIMBO WA ALI KIBA CHEKECHA CHEKETUA WAVUTIA MASHABIKI..... TAZAMAMA VIDEO
Sunday, March 08, 2015
VIDEO: MWAKYEMBE AWATAKA WASANII KUTOIMBA SIASA KWENYE NYIMBO ZAO
Wednesday, May 10, 2017