SERIKALI YA MISRI YAIMARISHA ULINZI KABLA MWAKA WA MASOMO KUANZA

Usalama waimarishwa kabla masomo kuanza Misri
Serikali ya Misri inayoungwa mkono na jeshi imeimarisha
hatua za usalama na za kiuendeshaji kabla ya kuanza mwaka mpya wa masomo nchini humo, kwa kuhofia maandamano ya wanafunzi wa sekondari na Vyuo Vikuu.

Miongoni mwa hatua nyinginezo, Cairo imeyafunga mabweni ya Chuo Kikuu cha al Azhar kama sehemu ya hatua zilizokusudiwa na serikali ili kuzuia uwezekano wa kutokea wimbi la maandamano chuoni hapo.

 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha al Azhar wanaopinga mapinduzi ya kijeshi wamesema kuwa hatua hiyo ya serikali inaonyesha kushindwa mamlaka za serikali.  

Maafisa wa serikali ya Cairo awali walitangaza kuwa kuanza mwaka mpya wa masomo kumesogezwa mbele kutoka Septemba 20 hadi Oktoba 11. 

Kuzana mwaka mpya wa masomo kumeakhirishwa huko Misri ikiwa umepita mwaka mmoja tu baada ya mamia ya wanafunzi kuuliwa, kujeruhiwa na kutiwa mbaroni katika ukandamizaji mkubwa wa serikali dhidi ya wafuasi wa Mohamed Morsi Rais halali wa Misri aliyepinduliwa na jeshi.