UINGEREZA KUPIGA KURA YA KUJIUNGA NA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS

Waziri Mkuu wa UINGEREZA, DAVID CAMERON

Waziri Mkuu wa UINGEREZA, DAVID CAMERON amesema nchi yake inajiandaa kwa kura muhimu kuhusu kujiunga katika mashambulizi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, IS. 

CAMERON amezungumza na mawaziri wake nchini UINGEREZA mara baada ya kutoka mjini NEW YORK, MAREKANI alikohudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Katika mkutano huo, kiongozi huyo amesema kuwa bunge la nchi yake litapiga kura IJUMAA, ili kuamua kama nchi hiyo inaweza kujiunga na mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini Iraq. 

Katika hatua nyingine polisi nchini UINGEREZA wamewakama watu 9, miongoni mwao akiwemo mhubiri shupavu wa Kiislamu ambaye anatuhumiwa kuwa na uhusiano na makundi yenye misimamo mikali.