UKRAINE, POLAND NALITHUANIA ZAKUBALIANA KUUNDA JESHI LA PAMOJA









Wanajeshi katika gwaride
Ukraine ,Poland na Lithuania zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja litakaloshirikisha maelfu ya wanajeshi.kijuzi.blogspot.com

Akizungumza baada ya mataifa hayo matatu kutia sahihi makubaliano hayo mjini Warsaw,rais wa Poland Bronislaw Komorowski amesema kuwa jeshi hilo linatarajiwa kufanya zoezi lake la kwanza la kijeshi mwaka huu na kwamba litashirikisha oparesheni za kulinda amani.
Kitengo hicho cha jeshi kitakuwa na makao yake makuu katika mji wa mashariki mwa Poland Lublin,ikiwa ni kilomita chache kutoka mpaka wa Ukraine.
Mpango wa Jeshi la pamoja ulianzishwa mnamo mwaka 2007 ,na sasa unaonekana kupigwa jeki na wasiwasi uliozushwa na jeshi la Urusi katika eneo hilo.