kijuzi.blogspot.com/uzi mpya wa man cityKLABU ya Manchester City imetoa jezi mpya za tatu zitakazotumiwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England katika michuano ambayo watashiriki msimu huu.kijuzi.blogspot.com/uzi mpya wa man city
Hii ndiyo jezi kamili mpya ya tatu ya Man City
Klabu hiyo inazindua jezi hizo kuelekea kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich Jumatano na zitatolewa rasmi kwa ajili ya mashabiki kuanzia Septemba 25.
Taarifa ya City kwa vyombo vya habari, imesema: "Chini ya wingu la kiza hizi jezi zinaonekana zinawaka, kama zinatiwa nguvu ya betri na zitatoa mwangaza fulani wa rangi uwanjani,".