VAN GAAL AFURAHIA UWEZEKANO WA RONALDO KUREJEA MANCCHESTER UNITED

RONALDO-FURAHA


























Louis van Gaal amesema yeye atafurahia kumrejesha Cristiano Ronaldo Manchester United lakini hadhani Real Madrid itamuuza.

Imedaiwa Ronaldokijuzi.blogspot.com ameonyesha nia ya kurudi tena Man United huku Rais wa zamani wa Real, Ramon Calderon, akidai Mchezaji huyo anataka aende Man United kwa sababu amechoshwa na Real kwa uamuzi wake wa kuwauza Mastaa wao ikiwa pamoja na Angel Di Maria ambae sasa yupo Man United.

Akiongea na Wanahabari kwenye Mahojiano kuhusu Mechi yao ya Jumapili ya Ligi Kuu England Ugenini na Leicester City, Van Gaal alijibu swali kwamba upo uwezekano wa wao kumchukua Ronaldo.

Van Gaal alisema: “Ndio lakini haya ni mazungumzo ya Magazeti na sidhani kama Vyombo vya Habari vitamnunua!”

Alipokazaniwa kujibu swali, Van Gaal alisema: “Inawezekana. Nilisema hivyo hivyo kwa Falcao. Wachezaji kama Ronaldo wanaleta mambo mengi kwenye Timu lakini sidhani kama Real watamuuza!”

Ronaldo, mwenye Miaka 29, alitwaa Mataji 8 akiwa chini ya Meneja Sir Alex Ferguson na Mwaka 2009 aliuzwa kwa Real kwa Dau la Rekodi ya Dunia kwa wakati huo la Pauni Milioni 80.

Mwezi uliopita, Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, alikiri angefurahia kurudi Man United pale aliposema: “Naipenda Manchester na huwezi kujua katika Soka. Ni kweli nina furaha hapa Real, ni nyumbani, ni Klabu yangu, lakini United walinitendea wema sana, na huwezi kujua!”

Aliongeza: “Bado nina mawasiliano na baadhi ya Watu huko kwa sababu nllikuwa na uhusiano mzuri na kila Mtu – ni kama Familia yangu ya pili!”