![]() |
| MEYA wa Jiji la MWANZA, STANSLAUS MABULA |
VIONGOZI wa riadha katika mikoa mbalimbali nchini wametakiwa kufufua mchezo huo ili uweze kutamba katika anga za kimataifa kama zamani.
Akizungumza baada ya kujisajili kushiriki mashindano ya ROCK CITY MARATHON, MEYA wa Jiji la MWANZA, STANSLAUS MABULA amesema viongozi wa mikoa wana wajibu mkubwa wa kuibua vipaji vya riadha na kuviendeleza katika maeneo yao.
Mashindano ya ROCK CITY MARATHON yanatarajiwa kufanyika jijini mwanza OCTOBA 26 mwaka huu kwa kushirikisha wanaridha wa ndani na nje ya nchi.

