WANAHABARI WATAKIWA KUFUTILIA TAARIFA ZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN
















Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN amewataka wamiliki wa vyombo vya baharini na taasisi zinazohusika na usafirishaji wa abiria na mizigo kujenga tabia ya kufuatilia miongozo ya wataalamu wa hali ya hewa ili kuimarisha usalama wa raia na mizigo yao wanaotumia usafiri wa vyombo mbalimbali vya baharini. 
DKT SHEIN amesema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani mjini UNGUJA na kusema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha maafa. 

Dakta SHEIN amesema Serikali ya Mapinduzi ya ZANZIBAR inatengeneza meli kubwa mpya itakayokuwa na uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na mizigo tani 200, huko Jamhuri ya Watu wa Korea inayotarajiwa kuwasili nchini mwezi MEI mwakani.