
Jeshi la Libya limeyataka makundi ya wanamgambo katika mji wa Benghazi kuweka chini silaha zao.
Msemaji wa jeshi la Libya Muhamamd Hijazi amesema kuwa, jeshi linatoa fursa ya mwisho kwa makundi yenye silaha yanayojishughulisha katika mji wa Benghazi kuweka chini silaha zao.
Ameongeza kuwa, iwapo makundi hayo hayatofanya hivyo jeshi litashambulia mji huo.
Msemaji wa jeshi la Libya aidha amesema, nchi hiyo inahitaji kukarabatiwa na makundi yenye silaha badala ya kuendeleza machafuko yanapaswa kuweka chini silaha na kushiriki katika ujenzi wa taifa.
Benghazi na Tripoli mji mkuu wa Libya, inahesabiwa kuwa miji yenye machafuko zaidi nchini humo, na Bunge la Libya limelazimika kuhamishia makao yake katika mji wa kaskazini mashariki wa Tobruk kwa sababu ya mapigano yaliyojiri hivi karibuni mjini Tripoli.