Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na DC Motema Pembe ya DRC, Mussa Hassan Mgosi dakika ya 16 aliyemalizia pasi ya kichwa ya Ame Ali na kumuwahi kipa Deo Munishi ‘Dida’ aliyetokea vizuri kutaka kudaka.
![]() |
| Kipigo cha kwanza; Kocha Marcio Maximo ameanza vibaya Ligi Kuu Bara |
Baada ya bao hilo, nyuki wakaingia uwanjani jambo lililosababisha wachezaji walale chini kwa dakika mbili, kabla ya wadudu hao kuondoka na mchezo kuendelea.

