ZAIDI YA WATU 300 WANUSURIKA KUFA MAJI

Watu 300 wanaodhaniwa kuwa ni wakimbizi kutoka nchini SYRIA wamenusurika kufa maji baada ya boti ya wavuvi waliokuwa wakisafiria kukumbwa na dhoruba na kupingwa na mawimbi makali katikati bahari.

Watu 300 wanaodhaniwa kuwa ni wakimbizi kutoka nchini SYRIA wamenusurika kufa maji baada ya boti ya wavuvi waliokuwa wakisafiria kukumbwa na dhoruba na kupingwa na mawimbi makali katikati bahari. 

Waziri wa ulinzi wa UGIRIKI amesema Kati ya wahamiaji hao haramu wengi wao walikuwa ni watoto na wanawake ambao walitelekezwa katika boti hiyo katikati ya bahari, hata hivyo watu wote waliokolewa na wako salama. 

Wahamiaji hao haramu walikuwa wakivuka mpaka katika bahari ya MEDITERANIANI kwenda kutafuta maisha nchi nyingine ikiwemo ITALIA na HISPANIA, UGIRIKI na CYPRUS ambazo zimekuwa zikitumiwa kama mlango wa wahamiaji kutoka AFRIKA na ASIA kuingia barani ULAYA. 

Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka huu idadi ya wahamiaji haramu kutoka nchini SYRIA wanaokimbia vita wamekuwa wakinusirika kifo na wegine kufa maji baada ya bodi wanazosafiri kuzidisha uzito