ZANZIBAR YARIDHIKA NA MCHAKATO WA KUFIKIA RASIMU YA KATIBA

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya ZANZIBAR Balozi SEIF ALI IDDI
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya ZANZIBAR Balozi SEIF ALI IDDI amesema ZANZIBAR imeridhika na namna hatua za Mchakato wa kufikia Rasimu ya Katiba inayopendekezwa ulivyofikiwa. 

Akizungumza na Vyombo mbalimbali vya Habari katika Ukumbi wa Spika Bungeni mjini Dodoma, Balozi SEIFF ALI IDD amesema kuwa Rasimu ya Katiba mpya inayopendekezwa imeingiza Hoja zote17 zilizowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, isipokuwa Hoja 4 ambazo bado zinafanyiwa kazi. 

Pamoja na kuridhishwa na Rasimu ya Katiba, Balozi SEIF amezungumzia suala la kujitoa kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar OTHMAN MASOUD OTHMAN kwenye Mchakato wa kupata Katiba mpya, akisema kuwa siyo kweli kwamba Mwanasheria huyo alishinikizwa kujitoa kwenye Kamati za Bunge.