AZAM FC YAWEKA REKODI MPYA LIGI KUU TANZANIA BARA

IMG_2655
KIKOSI CHA AZAM FC 2014/2015

Mabingwa watetezi wa Tanzania bara Azam FC leo imeweka rekodi mpya katika Vodacom Premier League baada ya kukamilisha idadi ya mechi 37 za ligi hiyo bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Azam FC leo hii walikuwa ugenini kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya walikuwa wakipambana na ‘Wajela Jela’ Tanzania Prisons.
Matokeo ya mchezo huo ni sare ya bila kufungana.
Azam FC msimu uliopita iliifikia rekodi ya Simba ya kumaliza ligi na kutwaa ubingwa bila kufungwa, na katika msimu huu mpya imeshinda mechi zake mbili za kwanza kabla ya leo kutoa sare na Prisons.