CCM wamaliza kikao cha kamati kuu kwa kuunga mkono Katiba inayopendekezwa
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi -NEC -
kimemalizika mjini DODOMA kwa kuunga mkono Katiba inayopendekezwa.
Pia NEC imewapongeza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa kufanikisha kupatikana kwa katiba hiyo inayopendekezwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini DODOMA, Katibu wa NEC wa
Itikadi na Uenezi, NAPE NNAUYE amesema kwa kiasi kikubwa, NEC imeunga
mkono katiba hiyo na kuwaomba wananchi kuikubali pindi itakapofika
wakati wa kupiga kura za maoni.
Kwa mujibu wa NAPE halmashauri kuu imepitisha kwa kauli moja sera ya kujitegemea kimapato na kiuchumi katika ngazi zote.