Akizungumza na tovuti ya Times Fm, Mpoto amesema ‘Ndovelwa’ ni jina linalotokana na lugha za kibantu za Tanzania na kwamba wimbo utakapotoka mashabiki wake watajua ni nini hasa anachomaanisha.
Mwimbaji huyo wa nyimbo nyingi za kijamii zinazolenga katika kuamsha zaidi wananchi na serikali katika masuala mbalimbali amesema kuwa kabla Diamond hajaingiza sauti kwenye wimbo wake, wamepanga kukutana na kufanya vikao seriously.
“Wakati nimezungumza na Diamond, tumezungumza kwamba atakapokuwa ametoka Canada, tarehe 1 October siku ya Jumatano, saa sita usiku. Itakuwa siku ya kwanza ya kuanza kurekodi hiyo ngoma. Kwa hiyo tutakuwa na kikao cha dakika 45 kwa mujibu wa maelezo yake tukijaribu kuwa katika same page, tukichambua yale mahudhui ya wimbo.” Mpoto ameiambia tovuti ya Times Fm.
Ameongeza kuwa tayari walishafanya vikao kadhaa kabla ya hivyo na kwamba lengo ni kuhakikisha wanapika kitu kikubwa zaidi kwa kuwa wote ni brand kubwa.
Usikose kusikiliza The Jump Off ya 100.5 Times Fm leo kuanzia saa mbili kamili usiku, Mrisho Mpoto atafunguka kwa urefu na kueleza mengi yaliyojiri baada ya kuachia ‘Waite’.