Dokta DAMAS NDUMBARO


WANASHERIA aliyeteuliwa na vilabu vya ligi kuu soka TANZANIA kusimamia kutokatwa makato yao na TFF , Dokta DAMAS NDUMBARO anakusudia kutafuta THELUTHI MBILI ya sahihi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho hilo kuelezea nia ya kutokuwa na imani na uongozi wa JAMAL MALINZI 

Katika kile kinachoonekana ni kuibuka kwa mgogoro wa kimaslahi kati ya vilabu hivyo na kamati ya utendaji ya TFF, DAMAS NDUMBARO ameorodhesha kwa kina jinsi ya TFF kutokuwa na sababu ya kukata mapato ya vilabu hivyo na kubainisha kuwa wataishtaki TFF au bodi ya ligi ikijiingiza katika makato ya vilabu hivyo. 

Aidha NDUMBARO katika taarifa yake yenye kurasa nane na hoja 27 amebainisha kwamba TFF iache wazo la kutaka kufanya makato hayo kwani kuna makato ya fedha kupitia FDF 

NDUMBARO kupitia vilabu hivyo wameionya TFF kutothubutu kuongeza makato yoyote kwani kufanya hivyo siku ya pili yake vilabu vya ligi kuu vitagomea michezo ya ligi hiyo ikiwa ni pamoja na kukataa udhamini kutoka kwa VODACOM na AZAM MEDIA 

Rais wa TFF, JAMALI MALINZI aliitaka bodi ya ligi kutii maamuzi ya kamati ya TFF hivyo ni lazima makato hayo yakatwe