
FIFA Leo hii imetangaza Majina ya Wachezaji 23 ambao ndio watakaogombea Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon d'Or, kwa Mwaka 2014 na miongoni mwao yupo Cristano Ronaldo ambae alitwaa Tuzo hiyo kwa Mwaka 2013.
Uingereza imetoa Mchezaji mmoja tu kwenye Listi hiyo ambae ni Gareth Bale wa Real Madrid lakini wapo Wachezaji watano wanaoechezea Klabu za Ligi Kuu England.
Wachezaji hao Watano ni Thibaut Courtois, Diego Costa, Angel Di Maria, Eden Hazard na Yaya Toure.
Miongoni mwa Listi hiyo ni Fowadi wa Barcelona, Lionel Messi, ambae ameshawahi kuitwaa Tuzo hii mara 4, ikiwa ni mara nyingi kupita yeyote.
Ronaldo, ambae anatarajiwa na wengi kuitwaa tena Ballon d'Or, anaongoza Wachezaji 6 kutoka Real Madrid wengine wakiwa Gareth Bale, Karim Benzema, Toni Kroos, Sergio Ramos na James Rodriguez.
Barcelona inao Messi, Neymar Junior, Javier Mascherano na Andres Iniesta.
Mabingwa wa Dunia Germany wanao Wachezaji 6 ambao ni Thomas Muller, Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger, Mario Gotze na Toni Kroos.
Listi hii ya Wachezaji 23 itapunguzwa na kubakia Wachezaji Watatu Mwezi Desemba na Mshindi atatangazwa Tarehe 12 Januari 2015 huko Zurich Nchini Uswisi.
Vile vile FIFA imetangaza Majina ya Mameneja 10 ambao watagombea Tuzo ya Meneja Bora na miongoni mwao ni Watatu kutoka Klabu za Ligi Kuu England ambao ni Jose Mourinho wa Chelsea, Luis van Gaal wa Manchester United na yule wa Man City, Manuel Pellegrini.
WAGOMBEA
Ballon d’Or:
-Gareth Bale
-Cristiano Ronaldo
-Karim Benzema
-Lionel Messi
-Thibault Courtois
-Eden Hazard
-Diego Costa
-Angel di Maria
-Yaya Toure
-Mario Gotze
-Zlatan Ibrahimovic
-Andres Iniesta
-Toni Kroos
-Philipp Lahm
-Javier Mascherano
-Thomas Muller
-Manuel Neuer
-Neymar
-Paul Pogba
-Sergio Ramos
-Arjen Robben
-James Rodriguez
-Bastian Schweinsteiger
Meneja Bora:
-Jose Mourinho
-Louis van Gaal
-Carlo Ancelotti
-Antonio Conte
-Pep Guardiola
-Jurgen Klinsmann
-Joachim Low
-Manuel Pellegrini
-Alejandro Sabella
-Diego Simeone