![]() |
Meneja wa Bia ya KILIMANJARO, GEORGE KAVISHE
|
BAADA ya TAIFA STARS kushinda mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya FIFA dhidi ya BENIN, wadhamini wa timu hiyo wamewataka wachezaji wa timu hiyo kuendeleza wimbi la ushindi ili TANZANIA siku moja iweze kung`ara katika michezo ya kimataifa.
Meneja wa Bia ya KILIMANJARO, GEORGE KAVISHE amesema ushindi huo mkubwa umewapa faraja na wapenda soka nchini.
TAIFA STARS ambayo ipo katika nafasi 115 katika viwango vya ubora vya FIFA iliichapa BENIN ambayo ipo nafasi ya 78 kwa jumla ya magoli MANNE kwa MOJA.